MAKADIRIO YA BEI
Unahitaji kitu tofauti? Pata makadirio ya bei.
Tuambie unachotaka kujenga, kuanzia tovuti au duka la mtandaoni hadi mfumo wa booking au app. Tunakujibu kwa makadirio yanayoonyesha kazi, muda na bei.
- Makadirio ndani ya siku 3 za kazi
- Punguzo hadi 25%
Tunaweza kukadiria bei ya
Kama mradi wako unalingana na kimoja cha vifurushi vyetu, unaweza pia kuchagua kifurushi moja kwa moja.
Ukurasa wa matangazo
Ukurasa mmoja kwa matangazo yako ya Instagram na Facebook, unaoishia kwenye mazungumzo ya WhatsApp.
Ona vifurushiTovuti ya biashara
Tovuti kwa Kiswahili na Kiingereza inayokusaidia kupatikana Google.
Ona vifurushiDuka la mtandaoni
Duka lako mwenyewe lenye malipo ya M-Pesa.
Ona vifurushiWeb app au mfumo wa biashara
Portal za wateja, dashibodi, booking, stoku na mifumo mingine inayoendana na jinsi unavyofanya kazi.
App ya simu
App za Android, iOS na web app zinazowekwa kwenye simu.
Kitu kingine
Kurasa au huduma zaidi ya kifurushi, mchanganyiko wa huduma, au wazo unalotaka tulijadili.
Jinsi inavyofanya kazi
Kutoka ujumbe wako hadi bei kamili.
Tuambie unachohitaji
Jaza fomu hapa chini au tuandikie WhatsApp. Mifano unayoipenda na kiwango cha bajeti yako vinasaidia.
Pokea makadirio yako
Ndani ya siku 3 za kazi unapata makadirio yenye kazi, muda na bei, kipengele kwa kipengele.
Thibitisha na tuanze
Makadirio yako yanaonyesha malipo ya awali ya kuanza na lini salio linalipwa. Mapunguzo yetu yanatolewa kwenye bei ya makadirio.
Tunajenga, unazindua
Tunajenga hatua kwa hatua na kukuonyesha kazi inavyoendelea.
Okoa hadi 25%
Mapunguzo yaleyale ya vifurushi vyetu yanatolewa kwenye bei ya makadirio yako.
- Punguzo la maoni
- 15%
- Punguzo kwa mteja wa mara ya kwanza
- 10%
- Unaokoa hadi
- 25%
Punguzo linatolewa kwenye bei ya kifurushi. Tutakuthibitishia mapunguzo yanayokuhusu kwenye makadirio ya bei yako.
Maswali kuhusu makadirio ya bei
Niombe makadirio lini badala ya kuchagua kifurushi?
Mradi wako usipoendana na kifurushi chetu: web app au mfumo wa biashara, app ya simu, kurasa au huduma zaidi ya kifurushi, au mchanganyiko wa huduma.
Makadirio yanachukua muda gani?
Unapata makadirio yako ndani ya siku 3 za kazi baada ya kutuma taarifa zako.
Mapunguzo yanahusu makadirio pia?
Ndiyo. Unapata punguzo la maoni (review) la 15%, pamoja na punguzo la 10% kama ni mteja wa mara ya kwanza: punguzo hadi 25% kwenye bei ya makadirio.
Niwatumie nini?
Unachotaka kujengwa na ni kwa ajili ya nani. Mifano ya tovuti au app unazozipenda, tovuti yako ya sasa au ukurasa wa Instagram, kiwango cha bajeti na muda unaouhitaji vinatusaidia kukadiria kwa usahihi.
Malipo yanafanyaje kazi?
Makadirio yako yanaonyesha bei, malipo ya awali ya kuanza na lini salio linalipwa. Tunaanza ukishathibitisha makadirio na kulipa malipo ya awali.
Pata makadirio yako ya bei
Tuma taarifa zako, tutakuandikia WhatsApp, kisha tutakutumia makadirio ndani ya siku 3 za kazi.
VIFURUSHI VYA BEI ISIYOBADILIKA
Je, mradi wako unafanana na mojawapo ya hivi?
Huna haja ya kusubiri makadirio: hivi vina bei isiyobadilika, muda maalum wa kukamilisha na punguzo zilezile.
Kurasa za matangazoUkurasa mmoja kwa matangazo yako ya Instagram na Facebook, unaoishia kwenye mazungumzo ya WhatsApp.Kuanzia TZS 250,000Ona vifurushi vya kurasa za matangazo
Tovuti za biasharaTovuti kwa Kiswahili na Kiingereza inayowasaidia watu wa karibu nawe kukupata Google.Kuanzia TZS 475,000Ona vifurushi vya tovuti za biashara
Maduka ya mtandaoniDuka lako la mtandaoni lenye malipo ya M-Pesa, ili uache kulinganisha screenshot za malipo na oda.Kuanzia TZS 1,500,000Ona vifurushi vya maduka ya mtandaoni



